Mastaa wa Bongo Fleva,Q-Chillah na TID mwishoni mwa wiki hii walitaka kutwangana walipokutana katika Klabu moja usiku.
Kwa mujibu wa Q-Chillah akizungumza kwenye Uheard na Soudy Brown alisema kuwa alikwenda kwenye klabu hiyo kuangalia shoo iliyokuwa ikifanyika lakini baadaye aliamua kutoka nje kucheza ‘pool table’ ndipo alipomuona TID.

‘’Nilimuona jamaa(TID) akiniangalia na baadaye
alinifuata akaniambia kuwa anataka kuongea na mimi nikamwambia ile siye
sehemu yake atafute muda mwingine ndiyo tuongee,’’alisema Q-Chillah.
Aidha Chillah aliongeza kuwa TID aliendea kumuongelesha
ndipo alimwambia kuwa anachofanya kumuongelea yeye vibaya siyo vizuri na
kile alichokipost hivi karibuni kuhusu kuuponda wimbo mpya wa msanii
Ali Kiba uitwao ‘Cheketua’ aliouachia hivi karibuni kupitia account yake
ya Instagram hakikuwa kitu cha busara ilitakiwa amsapoti kama msanii
mkongwe kuliko kumponda hadharani kupitia mitandao.
‘’Kiukweli kitendo cha TID kuandika Instagram kuwa ngoma mpya ya Alikiba ni mbaya na baada ya miezi mitatu haitokuwepo siyo kizuri nilimwambia yeye ni msanii mkubwa inabidi kumsapoti Ali Kiba na kwamba nilitaka kumpiga kwa fimbo ya pool table siyo kweli nilikuwa nikimueleza tu,’’aliongeza Q-Chillah.

Kwa muda mrefu wasanii hao wawili ambao waliwahi kuwa
pamoja kwenye bendi ya (Top Band) wamekuwa kwenye bifu zito wakitupiana
maneno kwenye vyombo vya habari.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment