Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa chama cha ACT-Wazalendo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Prof.Lipumba anadaiwa kukwepa
uzinduzi wa chama kipya cha siasa cha ACT-wazalendo. Uzinduzi wa chama
hicho umefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
leo 29 Machi 2015.
Aidha,Prof. Lipumba ni miongoni mwa wageni walioalikwa kutoa mada
katika uzinduzi wa chama cha ACT-Wazalendo kufuatia habari zilizotolewa
na chama hicho.
Hata hivyo wageni waalikwa kutoka nje ya nchi ambao ni Samia Nkrumah,
Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto wa Rais wa kwanza wa
Ghana, Osagyefo Kwame Nkrumah.
Wengine ni Ababu Namwamba-Katibu Mkuu wa Chama cha ODM cha Kenya;
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Kenya,
mabalozi wa nchi mbalimbali walioko nchini, kiongozi wa vyama rafiki
vya Ujerumani, Die Linke na Umoja wa vyama vya mrengo wa kushoto
Progressive Alliance nao hawaja hudhuria uzinduzi wa chama hicho.
Katika hatua nyingine wanachi mbalimbali walijitokeza kwa wingi kuhudhuria uzinduzi huo.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment