JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
29/03/2015
WATU 15 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA AKIWA HOSPITALINI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji
watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu
kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima ambaye amelazwa katika
Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Mnamo tarehe 29/03/2015 majira ya saa tisa na dakika thelathini usiku
watu hao 15 katika hali isiyo ya kawaida walifika hospitalini hapo
wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda kumuona mgonjwa huyo. Askari
ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia mashaka watu hao hivyo
waliwakatalia kuingia.
Kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia nguvu kuingia katika chumba
alicholazwa askofu Gwajima lakini walikamatwa na kikosi maalum cha
Polisi ambacho kabla ya tukio hilo walikuwa wanafuatilia mwenendo wa
kundi hilo.
Baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walipekuliwa hapo hapo TMJ na kukutwa
na Begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali kama ifuatavyo:
Silaha ambayo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu.
Risasi 17 za Shortgun.
Vitabu viwili vya Hundi (Cheque Books)
Hati ya kusafiria yenye jina la GWAJIMA JOSEPHAT MATHIAS yenye namba AB 544809.
Kitabu cha Hundi cha EQUITY Bank.
Nyaraka mbalimbali za kampuni ya PUMAChaja ya Simu na Tablets
Suti mbili na nguo za ndani.
Orodha ya watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
CHITAMA S/O MWAKIBAMBO, Miaka 32, Fundi Selemala, Mkazi wa Gongolamboto.
EDWIN S/O AUDEX, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Kawe Maringo.
ADAM S/O MWASELELE, Miaka 29, Mhandisi, Mkazi wa Kawe Maringo.
FREDERICK S/O FUSI, Miaka 25, Mkazi wa Mbezi Beach.
FRANK S/O JOHN MINJA, Miaka 24, Mwanafunzi IMTU, Mkazi wa Mbezi Beach.
EMMANUEL S/O NGWELA, Miaka 28, Mlinzi Shirikishi, Mkazi wa Keko Juu.
GEOFREY S/O WILLIAM, Miaka 30, Mhadhiri UDSM, Mkazi wa Survey Chuo Kikuu.
MATHEW S/O NYANGUSI, Miaka 62, Mchungaji, Mkazi wa Mtoni Kijichi.
BONIPHACE S/O NYAKYOMA, Miaka 30, Mchungaji, Mkazi wa Kitunda.
GEOFREY S/O ANDREW, Miaka 31, Dereva, Mkazi wa Kimara Baruti.
DAVID S/O MGONGOLO, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Ubungo Makoka.
GEORGE S/O MSAVA, Miaka 45, Mfanyabiashara, Mkazi wa Ilala Boma.
NICHOLAUS S/O PATRICK, Miaka 60, Mchungaji, Mkazi wa Mbagala Mission.
GEORGE S/O KIWIA, Miaka 37, Dalali wa magari, Mkazi wa Tandale Uzuri.
YEKONIA S/O BIHAGAZE, Miaka 39, Mchungaji, Mkazi wa Kimara Stop Over.
Baada ya upekuzi kukamilika watuhumiwa walifikishwa kituo cha Polisi cha
Oysterbay kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kupata uhalali wa wao
kumiliki silaha hizo na risasi mpaka walipokamatwa.
Upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa madhumuni ya kubaini sababu za
njama hizo sambamba na kujua mbinu zote zilizotumika kutaka kufanikisha
jaribio la kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment