Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mabinti Acheni Kuwakalia uchi waume za watu..Hawa Viumbe ni Wadhaifu Sana

Mabinti Acheni Kuwakalia uchi waume za watu..Hawa Viumbe ni Wadhaifu Sana


Jamani inasikitisha sana, pale binti anapoamua kutafuta mazingira tu na kuamua kumkalia uchi kwa makusudi kabisa mume wa mtu kwa lengo la kumpata, mkasa huu umetokea nyumba ninayoishi, kuna wapangaji vyumba vyao vipo karibu karibu, huyu mmoja ana msichana wa kazi, mwingine hana.

Huyu binti katafuta mazingira na kumkalia yule jamaa uchi kilichotokea ni yule jamaa kujikuta anaanza kumfuatilia msichana, na hali ukizingatia hakua hata na wazo na huyo dada na ni muda mrefu wanaishi hapo, kumbe dada na namba ya simu alishatafuta si ndo kuanza kuchati nae oh mpenzi sijui nini na nini.

Kindumbwe ndumbwe juzi wife wa jamaa kaona message, hapajakalika ugomvi na nyumba nzima wamejua. Jamaa akajitetea, ''Yaani mke wangu wala siko hivyo, na wala sina wazo na huyu mjinga, ila juzi tu nipo hapo uwani nafua nguo zangu si ndo akanikalia uchi, then badae ananitumia message tukachati, na wala sijui namba zangu kapata wapi''.

Aibu ndo hivyo tena!

Jamani mabinti acheni sio vizuri kumbuka hata na wewe utakuja olewa, kama unaona mwanaume haonyeshi muda na wewe muache na sio kumfanyia visa. Hawa viumbe 98% ni wadhaifu sana, Paja tu hoi, na nyie wanaume ukiona binti anakukalia uchi kama umetazama kwa bahati mbaya basi usigeuke tena potezea, hata binti atakuona una msimamo.

Asante kwa kuelewa.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips