Ben Pol amesema hayo kupitia Account yake ya Twitter ambapo amesema
msanii Diamond kishamfunga paka kengele na kilichobaki ni kuongeza nguvu
na kuona ni jinsi gani wanaweza kupenya zaidi na kuzidi kutanua mipaka
ya Bongo fleva ulimwenguni.
"Kiukweli Wanigeria Hawatuwezi Kimuziki,Na kuhusu Nani Atamfunga Paka kengele, Tayari Diamond Ameshamfunga Paka kengele"
Ben Pol amekuwa msaniii wa pili kuonyesha kuwa muziki wa Bongo fleva ni
muziki mzuri kuliko muziki wa Nigeria kwani hata msanii Mwanafalsafa
alishasema kuwa haupendi na haukubali kabisaa muziki wa Nigeria.Licha ya
baadhi ya wasanii kuusujudu na kuamini ndiyo muziki mzuri na ambao
wanahisi unapendwa sana kwa sasa lakini kwa Mwana Fa imekuwa tofauti
kwani alisema "Katika Habari nyingine,nimeamua kuwa hater wa mziki wa
Nigeria".
Kwa upande wake Diamond amezidi kushukuru Mungu kuona wimbo wake huo wa
Nitampata wapi unazdi kuchana mawimbi na kupokelewa vizuri hata nje ya
Afrika Mashariki kitu ambacho kinamfanya kujiona ni balozi mzuri zaidi
wa Afrika Mashariki.
"Asante Sana Mwenyez Mungu kwa Baraka zako zinazonifanya nizidi kuiwakilisha vyema Nchi yangu na Afrika Mashariki yangu..."
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment