BAADA ya kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho, raia wa Brazil, kuonyesha nia yake ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemkubalia lakini limempa masharti ya kufuata.
Coutinho aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu huu, alitamka kuwa kutokana na nafasi finyu ya yeye kuichezea timu ya taifa ya nchini kwao, basi yupo tayari kuichezea Taifa Stars kama TFF itamhitaji afanye hivyo.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema kuwa hakuna kifungu chochote ndani ya shirikisho hilo kitakachomzuia kuichezea Stars, lakini anatakiwa kwanza kubadili uraia na siyo shirikisho kuhangaika kumbadilishia.
“Sisi hatumzuii ila kama anahitaji hivyo inatakiwa yeye mwenyewe abadili uraia na siyo sisi kumbadili, kingine pia kocha wa timu ya taifa, Martin Nooij ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho kama akishabadili atutaarifu ili tufahamu, kama kocha akivutiwa na kiwango chake na akichaguliwa basi tumjumuishe kwenye kikosi,” alisema Mwesiga.
0 comments:
Post a Comment