Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mrisho Ngassa ajisalimisha Yanga Baada ya Tuhuma za Kutorokea Afrika Kusini

Mrisho Ngassa ajisalimisha Yanga Baada ya Tuhuma za Kutorokea Afrika Kusini

LICHA ya mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa,  kuwapigia simu viongozi wake juzi Jumanne, lakini wameahidi kuendelea kumchunguza kwa kuhusishwa na kutimkia nchini Afrika Kusini kwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, tofauti na alivyoomba ruhusa ya kushugulikia matatizo ya familia yake.

Wiki iliyopita Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha alikaririwa na Mwanaspoti kuwa alisikia Ngassa ametimkia Afrika Kusini na alipojaribu kumtafuta kwenye simu yake hakupatikana.

“Nimepigiwa simu na Ngassa usiku wa juzi Jumanne , tumezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kumuuliza maendeleo  ya matatizo ya familia yake, lakini hilo  halinifanyi   niache kuendelea kuchunguza ukweli juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake,” alisema.

Tiboroha alisema endapo kama itabainika  mchezaji wao kafanya kosa hilo atawajibishwa ili iwe mfano kwa wachezaji wengine kuzingatia nidhamu ya kazi zao za kufuata utaratibu unaotakiwa na siyo kufanya mambo kiholela.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips