Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na
Marehemu George Tyson, ameandika kwenye http://djchokamusic.com/ kwamba
Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa
madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni
Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka
tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka
kukaribia GAIRO mjini.
Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila
wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa
sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya
mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.
![]() |
![]() |
0 comments:
Post a Comment