Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » YALIYOJIRI NIGERIA: MSEMAJI WA P-SQUARE AONGEA KUHUSU TETESI ZA KUVUNJIKA KWA KUNDI

YALIYOJIRI NIGERIA: MSEMAJI WA P-SQUARE AONGEA KUHUSU TETESI ZA KUVUNJIKA KWA KUNDI




                                                                                                                                                          Wiki hii mitandao ya Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya mapacha wanaounda kundi la PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.

Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda ameachana na kundi hilo baada ya kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayofanyika Dubai.

Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo.

“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.” Alitweet Jude Okoye.

Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha habari hizo wakati akiongea na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi.

“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.” Amesema Bayo Adetu.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips