Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label Jacqueline Wolper. Show all posts
Showing posts with label Jacqueline Wolper. Show all posts

Hatimae Jacqueline Wolper Avishwa Pete ya Uchumba (Picha)

Mwezi mmoja toka Jacqueline wolper atamke kuwa ni mjamzito (ambao bado haujapata uthibitisho-Ingia hapa), mrembo huyo wa Bongo movie amevishwa pete ya uchumba.
wolper-5
Kwa mujibu wa picha na maelezo aliyopost kwenye akaunti yake ya Instagram, Wolper sasa ni mchumba wa mtu.
wolper-2
wolper-3
wolper-4
Wolper alipost picha kadhaa akiwa na mchumba wake, na kuelezea picha kamili ilivyokuwa hadi kupata surprise hiyo ambayo hakuitarajia.
wolper insta
Baada ya maelezo hayo yaliyofatiwa na picha za tukio lenyewe, pongezi nyingi zimemwagika kutoka kwa followers wake. Hizi ni baadhi ya comments;
annietzdu: Nakupongeza kwa kutochukua mtu maarufu mungu awatangulie sana mtimize lengo lenu mmeendana sana
new_isha: Usiishie Pete ndoa fastaaa my nduguuuu love uuuu na unialike
mwezimbili: Hongera kaka kwan umembadilisha tabia Dada Jack.hususanani ktk mavazi Mungu amibariki.Dada Jack jitambue kuna ile SKU moja utakua mama hivyo basi heshima ndio nguzo pekee ktk masha hebu onyesha mfano.
beibycso: Aya akuoe ss mn asije akw bongo movie na yy. Me nshakataaga mambo ya pete n nini stak we njoo toa mahar nioe ful stop stak aibu mjn wanaume hawatabirikiiiii

hotkipepeo: All the best sina shaka na wewe hata ukifunga ndoa una vielement vya umama bora ukawe hvyo hvyo ruwa nakutarame
3

Jack Wolper Amchana Laivu Chuchu Hans..Kisa Siasa

SIASA katika ubora wake! Nyota wa filamu nchini, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’ amemchana staa mwenzake, Chuchu Hans kufuatia kutofautiana kiitikadi kisiasa kati ya chama tawala (CCM) na Ukawa.


Awali, Chuchu Hans alitangaza kuhamia Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) na kushiriki kikamilifu kwenye uzinduzi wa kampeni zao uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, Dar wiki iliyopita.

Lakini ghafla, Chuchu alionekana akiwa amevaa sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutangaza kwamba ameamua kurudi nyumbani, kitendo kilichoonekana kumkera mno Wolper, ambaye amejipambanua kuwa ni mfuasi namba moja wa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

“Sijui huu uzalendo wa Tanzania utakuja lini, yaani wewe juzi tuwe wote na sare uvae, leo umetusaliti kisa vijisenti sasa aliyekwambia Ukawa tunapewa hela ukaja na mbwembwe zote nani? Sikuwa na lengo la kukuweka hapa ila nataka niseme kitu kimoja, jamani hamna kitu kibaya kama unafiki, tamaa na njaa, hii ni nchi yetu sasa tukihongwa wote ili tuwe chama kimoja ukombozi utakuwa wapi,” ilisomeka sehemu ya waraka ambao msanii huyo aliuweka katika mtandao wake wa Instagram.


Gazeti hili lilimtafuta muigizaji huyo ambaye ni mpenzi wa Vincent Kigosi ‘Ray’ na alipotakiwa kuzungumzia jambo hilo, alifunguka:

“Sikutaka kujibu, lakini nimwambie Wolper ingawa mimi nimewahi kuzaa, lakini yeye ni dada yangu, kanizidi umri, kwenye siasa kila mtu ana haki ya kupenda kule anakotaka mwenyewe. Ni kweli nilienda Ukawa, lakini baadaye nikagundua hawana ‘ishu’ nimerudi zangu CCM.”
Source:Globalpublishers 3

Jacqueline Wolper ana mimba ya miezi mitatu? ‘Mine is on the way 5 months to go’

Jacqueline Wolper ni mama kijacho – at least kwa maneno yake mwenyewe aliyoandika Instagram wakati akiwapongeza Diamond na Zari kwa kupata mtoto wao wa kwanza, Latiffah.

Congratulations dad and mom MTV, God is always great, Congrats Wasafi President for the little princes. Mine is on the way 5 months to go!!,” ameandika Wolper.

“Sema mtoto wa kwanza bwana unaweza kujikuta unataka kum’beba wewe tuu na kazini usiendee, utunyime mashabk haki yetu ukaacha kututungia viburudisho ukawa unalea. Hongera mtani wangu one love @diamondplatnumz,” ameongeza.

Tusubiri kama taarifa yake ina ukweli!
3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips