Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label Augustine Mrema. Show all posts
Showing posts with label Augustine Mrema. Show all posts

Mrema Ajitokeza Kwa Mara Nyingine Tena Kumkumbusha Rais Magufuli Ampe Kazi Yoyote

Mwenyekiti wa TLP taifa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesisistiza ombi lake la kazi kwa kumkumbusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwamba ampe kazi yoyote amsaidie kibarua kigumu alichonacho cha kuwahudumia wananchi

Dkt. Mrema ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine ambaye alihudumu kwenye awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Nyerere ambapo alifariki akiwa na cheo cha waziri mkuu tarehe 12.04.1984 kwa ajali ya gari.

''Namkumbuka Sokoine kama mtu wa watu aliyehudumia watu, aliyepambana na ufisadi na magendo .Alikuwa anatenda haki kwa wananchi wote .

"Hata mimi nilipokuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu nilijaribu kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa kama yeye kwa sababu sikuwa waziri mkuu au Rais''- Alisisistiza Mrema.

Kuhusu Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli
Mrema alisema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi wa  Rais Dkt. Magufuli, aliwahimiza wananchi wa Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia wananchi wa Vunjo kwamba Mrema akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo hiyo wananchi wanaulizia.

Aidha Mrema alisema kuna maeneo ambayo yeye anafiti siyo lazima apewe madaraka makubwa

"Mimi sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri, anipe kazi yoyote na nikionana naye nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu." Alisema Mrema

Hata hivyo Dkt. Mrema alimpongeza Dkt. Magufuli kwamba ni mtendaji ambaye ameamua bila kusukumwa kupambana na mafisadi na kwamba yeye ni alfa na omega na kazi hiyo ameonyesha kwamba atafanya vizuri kuliko Sokoine na Mrema. 3

Augustine Mrema Ndio Basi Tena ..Mbatia atwaa Vunjo, Komu mshindi Moshi Vijijini

By auli Giliard/Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Tume ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza James Mbatia wa NCCR Mageuzi kuwa mbunge mteule wa jimbo la Vunjo huku kada wa Chadema, Anthony Komu naye akiibuka mshindi katika jimbo la Moshi Vijijini lililokuwa linaongozwa na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Dk. Cyril Chami kupitia CCM.

Akitangaza matokeo ya majimbo hayo mawili mkoani Kilimanjaro kuamkia leo, msimamizi Fulgence Mponji, amesema Mbatia amepata kura 60,187 akiwashinda wapinzani wake; Innocent Shirima wa CCM aliyepata kura 16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 6,416.

Kutokana na matokeo hayo,  Mrema ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo huku wananchi wa eneo hilo wakiendeleza historia ya kutomchagua mbunge wa chama kimoja kwa vipindi viwili tangu kurudi kwa mfumo wa siasa za vyama vingi.

Kwa upande mwingine, CCM imepoteza jimbo la Moshi Vijijini kupitia kwa mgombea Cyril Chami na kurudi tena upinzani baada ya kada wa Chadema, Anthony Komu kutangazwa mshindi. Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa Viwanda na Biashara hakuwepo wakati NEC wa kusaini kuonyesha kuwa amekubali matokeo.

Kwa mujibu wa Mponji, mbunge mteule wa Moshi Vijijini, Komu amepata kura 55,813 huku Dk Cyril Chami akijikusanyia kura kura 24,415.


Quote: What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions disappointed, investments won, investments lost, elections won, elections lost - these things may occupy our attention, but they do not define us. By Mitt Romney 3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips