Fredrick Sumaye |
Kwa mujibu wa Sumaye, fedha hizo ambazo Serikali ya CCM imeshindwa kuzirudisha zitatakiwa kurudi kwa sababu ni mali ya Watanzania.
“Jana (juzi) mmemsikia Magufuli (Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli), akisema atakapoingia madarakani atarudisha mashamba ya wananchi yaliyoporwa.
“Kwanza kabisa namwambia Magufuli kwamba Ikulu haingii, lakini sisi tutakapoingia madarakani tutahakikisha walioiba fedha za Watanzania na kuzificha huko Ulaya au Uswisi wanazirudisha,” alisema Sumaye.
Sumaye pia alizungumzia suala la rushwa nchini na kusema kama CCM wangekuwa waungwana wasingemsimamisha mtu yeyote kugombea urais kwa sababu wameshindwa kuwaletea maisha bora Watanzania.
“Magufuli anasema akiingia madarakani atakomesha rushwa sasa kama ana uwezo huo kwa nini ameshindwa kuikomesha wakati na yeye ni waziri katika Serikali iliyokithiri kwa rushwa?
“Magufuli anasema akiingia madarakani atakuza uchumi, kama kweli ana uwezo wa kukuza uchumi kwa nini ameshindwa kuukuza kupitia Serikali ya CCM ambayo yeye ni waziri?
“Magufuli hana lolote, msimchague kwa sababu ameshiriki kununua feri mbovu inayotoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam,” alisema Sumaye.
Katika maelezo yake, Sumaye alizungumzia pia taarifa za viongozi wa CCM wanaodaiwa kuwatisha wananchi wasimchague Lowassa kwa kisingizio kwamba nchi itaingia katika vita kama ilivyotokea Libya na katika nchi nyingine za Afrika Kaskazini.
Sumaye alisema hakuna vita itakayotokea wapinzani watakapoingia madarakani na kwamba vita hiyo itatokea kama Serikali ya CCM haitataka kuondoka madarakani. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment