Ghafla Mkurugenzi huyo ameamua kujitoa kwenye timu hiyo baada ya kuona anapoteza nguvu zake wakati ana uhakika wa 100% kuwa Magufuli ndiye Rais wa awamu ya tano. Mengi amesema haoni faida ya kupoteza muda wake kumuunga mkono mtu mwenye uhakika wa kushindwa. Mengi amekubali wazi kuwa ushindi wa kiti cha Urais 2015 ni wa Magufuli... "kama hawa jamaa watashinda nafasi ya Urais basi ni baada ya miaka 10 siyo hivi sasa, huu mwaka ushindi utakuwa wa Magufuli tu tutake tusitake"
Pigo kubwa kama hilo limeambatana na kuondoka kwa wasanii mbalimbali waliotimkia kambi ya Ndugu Magufuli akiwemo Aunt Ezekiel, Ray na Juma Nature. Mshirika wake mkuu Hussein Bashe nae amejiweka pembeni na kuutangazia umma kuwa "ili wananchi wawe salama ni lazima kiti cha urais kikabidhiwe kwenye mikono salama, kinyume chake wananchi hawatokuwa salama, na mikono salama ni ya ndugu Magufuli tu"
Mwaka wa kufa nyani miti yote huteleza, EDO keshaanza kufa na miti yake pia imeanza kuteleza taratibu
0 comments:
Post a Comment