Sumaye alisema wamezunguka maeneo mengi ya nchi kila walipokuwa wakienda wamebaini Watanzania hivi sasa wanahitaji mabadiliko na hawana mpango wa kuongozwa tena na CCM.
Aidha Sumaye alipingana na wale wanaosema amejiunga Ukawa kwa uchu wa madaraka, na kusema kuwa uchu wake wa kujiunga Ukawa ni kutaka kuing’oa CCM.
“Sikuja UKAWA kutafuta cheo kwa sababu nimeshakuwa waziri mkuu na hata hapa Ukawa hakuna nafasi ninayotaka kwa sababu nafasi ya urais yupo Lowassa na nafasi ya waziri mkuu siwezi kupata kwa sababu sijagombea ubunge ila ninachofanya ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani,”
Sumaye alisema kwa kuingia kwake UKAWA, amejikuta akipata vitisho kutoka serikalini:.
“Suala la kunitisha kuninyang’anya mashamba yangu ni kunikomaza zaidi kwa kuwa naamini suala hilo ni sawa na kumpiga chura teke.” WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment