Wacha tusemezane kidogo...na leo tusemezane juu ya hii silaha ya maangamizi ya ndugu Lowassa.
Ikiwa Lowassa na Mbowe wataweza kuhakikisha Slaa anaendelea kunyamaza, nini itakuwa athari kwa mbio zao kuelekea Magogoni? Hii itaendelea kuwaaminisha wale walioamua kufa kishujaa na Slaa na wale ambao bado hawajaamua nani wampigie kura waendelee kuamini kuwa Lowassa ni Fisadi na hafai kuwa Amiri Jeshi wa Majeshi yetu.
Ila Mbowe na Lowassa endapo watazichanga karata zao vizuri na kumuangukia Slaa na Slaa hata akaamua kushiriki katika Campaign japo kishingo upande, basi CCM wategemee upinzani mkali ambao hawajawahi kuupata tangu kuzaliwa kwa chama hicho.
Ila endapo Mbowe na Lowassa wakampuuza Slaa kwa kuamini kwamba hana impact yeyote eti kisa tu watu wanataka Mabadiliko, basi endapo Slaa ataamua kuufungua mdomo wake kuongea na Watanzania, Mbowe na Lowassa wategemee anguko kuu ambalo halijawahi kuonekana katika nchi hii.
Tujaribuni kusemezana kistaarabu tu, kama Mbowe na Lowassa wanavyohubiri namna Campaign zitakavyoendeshwa bila ya matusi, basi na hapa tusemezane tu bila Matusi.
0 comments:
Post a Comment