Hemedy amesema kuwa yeye ni shabiki mkubwa sana wa Drake, na ndiye msanii wa nje anayemu-inspire kwa kiasi kikubwa ndio sababu huwa anampost sana kwenye akaunti zake lakini sio kwasababu anajifananisha naye.
“Ninamkubali sana drake lakini sijifananishi na Drake” alisema Hemedy kupitia Clouds’E’ ya Clouds TV.
Lakini kama kawaida yake hakuacha kujifagilia kidogo, kwa kusema kuwa licha ya kumpenda Drake lakini bado yeye (Hemedy) anamzidi Drake mambo mengi ikiwemo muonekano wake na kuvaa.
“Nina muonekano mzuri kuliko Drake, navaa vizuri kuliko drake” – Hemedy PHD
Hemedy ambaye hivi karibuni ameachia video mpya ‘Imebaki Story’, pia amezungumzia maana ya ‘Papi Nation’ kuwa ni jina la kampuni yake anayotarajia kuisajili hivi karibuni.
BONGO 5
0 comments:
Post a Comment