Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mrema asema UKAWA umepoteza mwelekeo

Mrema asema UKAWA umepoteza mwelekeo

Mwenyekiti wa taifa wa TLP Augustine Mrema amewatahadharisha watanzania kuwa macho juu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umepoteza mwelekeo na kuyumba kisiasa na kudai kuwa hawafai kuingia ikulu na kuongoza nchi.

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP , Augustino Lyatonga Mrema
Mrema ametoa tahadhari katika eneo la njiapanda baada ya kurejea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Moshi kuchukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo huku akisindikizwa na wafuasi wake.
Amesema, kitendo cha ukawa kumkashifu hadharani waziri aliyestaafu Mh
Edward Lowasa kuwa ni fisadi na baadaye kumpokea na kumteua kuwa mgombea wa urais ukawa imeonyesha udhaifu mkubwa na kwamba watanzania wa sasa si wakuburuzwa.
Mh. Mrema amesema kuwa haiwezekani mtu alieachwa na chama na kuonekana hafai kutokana na tuhuma za ufisadi kicha CHADEMA ndio wakaona anafaa kuwa mgombea huko ni kuonyesha kutokuwa na msimamo ndani ya hivyo ni vigumu kuwapa uongozi wa nchi. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips