Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Majimbo Matano Kurudia Kupiga Kura za Maoni CCM

Majimbo Matano Kurudia Kupiga Kura za Maoni CCM

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) imeagiza kurudiwa kwa uchaguzi katika majimbo matano yaliyopo Tanzania Bara kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika mchakato wa kura ya maoni.

Majimbo yanayotakiwa kurudia uchaguzi wa kura ya maoni ni pamoja na Makete, Busega, Ukonga, Rufiji na jimbo la Kilolo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema mchakato huo utarudiwa siku ya Alhamisi Agosti 13 mwaka huu.
Amesema baada ya uchaguzi huo matokeo yatapelekwa katika vikao vinavyoendelea kwa ajili ya uamuzi.

Akizungumzia kuhusu vikao vinavyoendelea katika ukumbi wa NEC mjini Dodoma amesema vikao hivyo vinaendelea vizuri ambapo jana kikao cha kamati ya maadili kiliendelea mpaka usiku.
Amesema leo wanatarajia kumaliza kikao cha Kamati Kuu ambapo kesho na kesho kutwa watamaliza na kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho (NEC) kama ilivyopangwa. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips