Headlines zilizonifikia muda huu zinatoka Austria ambako maiti za wahamiaji 71 zimekutwa ndani ya lori lililotelekezwa kwenye njia panda ya barabara.
Vyombo vya habari kutoka Austria vinasema kuwa lori hilo liligunduliwa na baadhi ya polisi waliokuwa kazini kwenye njia panda ya Austrian Highway mida ya asubuhi na polisi hao wanasema lori hilo lilikuwa limetoka Hungary kueleka Austria.
Wakizungumza na vyombo vya habari, Polisi walisema kuwa walipokaribia lori hilo walisikia harufu kali ya kitu kuvunda ndipo kufungua nyuma ya lori hilo na kukuta maiti ya wahamiaji 71 ikivunda kutokana na joto kali lililokuepo ndani ya lori hilo… kati ya hao 71 polisi wanasema, 60 ni wanaume , wanawake 8 na watoto 3 wenye miaka 2,3 na 8.
>>> “Hawa walikuwa wanajaribu kuingia nchini kwani mwisho wa hii highway ni mpaka unaonganisha mji wa Budapest, Hunary na mji mkuu wa Austria, Vienna… hatuna uhakika sana ila inatulazimu kuamini kuwa hawa ni wahamiaji, kwani kuna sababu gani nyingie ya watu wote hawa kujiificha ndani ya lori hili kama walikuwa hawajaribu kuvuka mpaka?” <<< Peter Doskozi, Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Austria Burgenland.
Peter Doskozi aliongeza kwa kusema kuna karibia malori 3,000 yanayopita highway hio kila siku kitu kinachofanya ukaguzi wa malori hayo kuwa kazi ngumu na watu wengi wanaojaribu kuingia nchini humo kwa njia zisizo halali hutumia magari madogo na wale wachache wanaotumia malori hawakaguliwi hivyo ni vigumu kuwapata.
0 comments:
Post a Comment