Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Hatimaye UKAWA Wakubaliwa Kutumia Uwanja wa Jangwani Jumamosi hii Kuzindua Kampeni zao

Hatimaye UKAWA Wakubaliwa Kutumia Uwanja wa Jangwani Jumamosi hii Kuzindua Kampeni zao

Lowassa Akizungumza na Wahandishi wa Habari
Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na  taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene zimesema kuwa uzinduzi huo utafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.

Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama  vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia  nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa  serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema  hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za  CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma  na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa  malalamiko yao. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips