Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , » Hatimae Polisi Kutoa Tamko CCM Kuzidisha Muda wa Kampeni Baada ya NEC Kudai ilikuwa Kazi yao Kuwazuia CCM

Hatimae Polisi Kutoa Tamko CCM Kuzidisha Muda wa Kampeni Baada ya NEC Kudai ilikuwa Kazi yao Kuwazuia CCM


Kamishna wa operesheni mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Paul Chagonja
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema kuwa litatoa tamko la jeshi hilo juu ya Chama cha Mapinduzi kuzidisha muda wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za chama hicho wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa wadau wa uchaguzi leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Mafunzo na Operasheni wa Jeshi la Polisi CP Paul Chagonja amesema kuwa wanashughulikia suala hilo na muda ukifika watatoa tamko.
Ameongeza kuwa ili uchaguzi uwe wa Amani ni lazima watu wote watimize wajibu wao.
Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwakilishwa na Jaji Mstaafu John Mkwawa amevitaka vyama vya siasa kuzingatia maadili ya uchaguzi waliosaini ili kulinda amani na kuepusha migogoro na uvunjifu wa Amani.
Kwa upande wa mwakilishi toka chama cha ADC Mwanaisha Yemba amevitaka vyama vyenye vikundi vya ulinzi kuwapa sare na alama maalum walinzi wao ili watambuliwe na kila mtu ili wakifanya vujo iwe rahisi kutambulika. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips