Chris Brown ana sababu nyingi za kusherekea weekend hii na starehe zote za dunia, siku ya Alhamisi (tarehe 27 August) staa huyu wa muziki wa R&B Pop alichukuwa time na kupost kwenye page yake ya Instagram tuzo ama pongezi aliyopewa na lebo kubwa ya muziki RCA Records ya Marekani.
Pongezi hiyo iliyotolewa kwake na lebo ya RCA Records ilihusisha vitu 3; pongezi ya mauzo yake kimuziki za Album miliion 10, pongezi ya mauzo ya single zake zinazozidi milllion 60, pongezi kwa tuzo 14 za BET, pongezi kwa nyimbo 19 zilizoshika #1 na pongezi kwa kuwa miongoni mwa wasanii wadogo duniani wenye watazamaji zaidi ya Billion 3.5 kwenye channel yake ya YouTube!
Nadhani utakubaliana na mimi kuwa licha ya matatizo na headlines tofauti anazoweka Chris Brown mitandaoni, msanii huyu wa miaka 26 ni miongoni mwa wasanii wadogo wenye ushawishi mkubwa sana duniani na pongezi hii inathibitisha kwa kiasi gani!
Niliweza kuzinasa hizi post mbili kupitia page yake ya Instagram @chrisbrownofficial.
Big up sana kwa mtu wetu Chris Brown!
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment