Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Nampa Kila Anachostahili Mke Wangu Lakini Sina Amani na Ndoa yangu....

Nampa Kila Anachostahili Mke Wangu Lakini Sina Amani na Ndoa yangu....

Mke wangu nampenda sana kila anachotaka nampa. Yeye ni mwalimu wa msingi. Uwezo wangu wa kifedha si mkubwa lakini nimejitahidi hadi nimemnunulia walau kigari cha kuendea kazini katika jitihada za kumfanya nae ajisikie vizuri mbele za watu.

Mshahara wake ni chini ya laki 5 lakini huwa namwekea mafuta ya shilingi laki 3 kwa mwezi ili aende kazini. Nampa matunzo yote anayotaka kama mke wa ndoa anavyostahili.

Kinachonisikitisha ni dharau anazonionyesha ndani ya nyumba. Akiamua kunitukana inachukua siku tatu kumaliza matusi. Nyumba haina amani naishi kama mhamiaji haramu. Kuna wakati ananiangalia tu na kunisonya bila kumkosea chochote.

Anadai nikisafiri anaishi kwa amani nikirudi anakereka. Kwa kifupi mimi huwa ni mara chache huwa najibizana nae ninapozidiwa na hasira lakini mara nyingi hukaa kimya.

Nimejaribu kujiuliza ni wapi nakosea sipati jibu. Natunza familia vizuri, unyumba nampa, sina vimada na wala hajawahi kunihisi.

Tatizo ni nini? Nisaidieni wadau niishije na huyu mke? Akiugua anajitahidi kuonyesha jamii kuwa simjali anaamka mapemaa anawahi hospitali ili nionekane simjali.

Akiamua kunitukana anatumia matusi na kashfa nzito dhidi yangu. Bado sijamsimulia mtu yeyote kwa ajili ya kulinda heshima ya familia lakini naona kama nazidiwa.

Naombeni ushauri wenu. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips