Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » LOWASSA Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais LEO kwa Mbwembwe na Shamrashamra!!

LOWASSA Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais LEO kwa Mbwembwe na Shamrashamra!!

Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alitambulishwa rasmi kuhamia CHADEMA July 28 2015 Dar es Salaam akiwa ameongozana na mke wake, Regina Lowassa pamoja na watoto wao.

Kwenye Orodha ya Viongozi wa UKAWA ambao walikuwepo kumpokea na kumkabidhi kadi ya CHADEMA, alikuwepo James Mbatia, Prof. Lipumba, Dk. Emmanuel Makaidi, Salum Mwalimu na Freeman Mbowe.

Salum Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, jana  alisema haya kuhusu mapokezi hayo;

"Tunashukuru sana Watanzania, sidhani kama kuna kiongozi wa CHADEMA simu yake iliwahi kuzidiwa kama jana, simu zilizidiwa kwa pongezi… Kila mtu amezungumza kwa sababu ya Historia ya tendo lenyewe.

"Kesho(LEO) Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA… pengine kutakuwa na shamrashamra nyingi itategemeana na Mgombea mwenyewe, akiamua kuja na mdundiko haya… lakini tunaamini kutakuwa na shamrashamra nyingi."

Salum Mwalimu pia  alizungumzia  sababu  za  viongozi  wengine  wa  UKAWA  kutokuwepo(  Tundu Lissu  na  Dr. Slaa)   ambapo  alisema;

"Tuna mambo mengi tuna mikakati mingi, tumegawanyika… sio kila tukio wote tuwe pamoja.

"Jana mliuliza Tundu Lissu yuko wapi na leo huyu hapa hata hamumuulizi… Tuko kwenye kipindi cha Uchaguzi,tuna mambo mengi hatuwezi wote kuwa sehemu moja, tunagawanyika kutokana na ratiba tuliyonayo." WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips