Bastian, mwenye umri wa miaka 30, aliomba mwenyewe klabu ya Bayern Munich kutompa mkataba mpya na angependa kwenda sehemu nyingine.
Mkurugenzi mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge ameongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita na kusema: “Marafiki zangu wa pale Manchester United tumekuwa na mawasiliano kwa muda kidogo. Tumefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Bastian.
Schweinsteiger ameshaichezea Bayern Munich mechi 536 tangu alipovaa jezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2002.
Inamaanika kwamba Bastian amevutiwa kujiunga na Manchester United kutokana na kuwa na mahusiano mazuri na kocha Louis van Gaal ambaye alimfundisha soka wakati alipokuwa kocha wa Bayern Munich.
Ada ya uhamisho iliyolipwa kumsajili Schwesteiger inaaminika kuwa karibia kiasi cha £8m na mshahara wake utakuwa kiasi cha £7m kwa mwaka.
Kwa kujiunga na Man United Bastian Schwesteiger anakuwa mchezaji wa kwanza wa kijerumani kuitumikia Manchester United.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment