Na
taarifa ikufikie kwamba Airtel Rising Stars imerejea tena kwenye
headlines na itatambulishwa rasmi Jumatano ya 17 June 2015 Dar es Salaam
ikiwa inasimamiwa na kampuni hii inayoongoza kwa ubora katika nchi 20
za Asia na Afrika.
Airtel Afrika imemtangaza rasmi Yaya Toure
kuwa balozi mpya kwa ajili ya kampeni mpya itayotambulishwa Afrika
ambapo ushirikiano kati ya Airtel na kapteni huyo wa Ivory Coast na
kiungo wa Manchester City utaanza rasmi katika uzinduzi wa kampeni mpya
ya “It’s Now” yenye lengo la kulea na kukuza vipaji barani Afrika.
Ni kukuza vipaji kupitia nyanja mbalimbali
kama vile michezo, ikijumuisha mashindano ya Airtel Rising Stars kwa
vijana chini ya umri wa miaka 17 ambayo mwaka huu yanatarajiwa Dar es
Salaam, Jumatano, Juni 17 sehemu nyingine ambazo kampeni hii itazigusa
ni kama vile mfumo mzima wa maisha na muziki ambapo wateja watapata
ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kiteknolojia ili kuona fursa
zinazowazunguka.
Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Afrika,
Christian de Faria amesema hii kampeni inadhihirisha nia ya dhati ya
kampuni ya Airtel katika kuwaunga mkono vijana wa Afrika pia na kukuza
fursa mbalimbali za kiuchumi.
Akizungumzia ushirikiano wake na Airtel,
Toure amesema, “katika kipindi chote ambacho nimetumika katika tasnia ya
soka, nimekuwa ni mwenye bahati kubwa sana kupata mkataba huu kutokana
na mafanikio niliyoyapata uwanjani, hata hivyo, najua kwamba
unawezakucheza katika kiwango cha juu endapo utajitolea kwa asilimia 100
uwanjani. “It’sNow” ni kampeni ambayo ipo moyoni mwangu kwani inalenga
kuwaamsha vijana wa Afrika kuchangamkia fursa zinazowazunguka ili kuwa
na maisha bora.
Ninajivunia sana kufanya kazi na Airtel
ambayo inafika maeneo mengi ya Afrika ili kuwapa ari vijana watu wengi,
Kwa upande wake, Colaso alisema, “Kwetu sisi hapa Tanzania kampeni hii
ya It’s Now inaenda bega kwa bega na progamu ya Airtel Fursa ambayo
ilizinduliwa mwezi Mei mwaka huu, pamoja na Airtel Rising Stars ambayo
inatarijia kuanza wiki hii. Tuna imani kubwa kuwa vijana wetu hapa nchini watakuwa na ari kubwa kutokana na uwepo wa Toure katika kampeni hii itakayojumuisha masuala ya michezo, maisha pamoja na muziki.
inatarijia kuanza wiki hii. Tuna imani kubwa kuwa vijana wetu hapa nchini watakuwa na ari kubwa kutokana na uwepo wa Toure katika kampeni hii itakayojumuisha masuala ya michezo, maisha pamoja na muziki.
Tunawaasa vijana wenye nguvu na nia ya
dhati kuikimbilia fursa hii ili kujikwamua wao wenyewe pamoja na familia
zao, ushirikiano huu utampelekekea Toure kuunga mkono shughuli za
kijamii hasa kuwawezesha vijana kupata maendeleo.
Ikiwa imeingia barani Afrika tangu mwaka
2010, Airtel Afrika imekuwa ikijiongezea wateja kufikia zaidi ya watu
milioni 70.Kwa sasa Airtel ndio kampuni inayoongozwa kwa huduma bora za
internet aina ya 3G katika nchi 17, huku pia ikitoa huduma z kifedha kwa
njia ya simu za Airtel Money.
Gallos Official Blog
Chanzo millard ayo.com
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Chanzo millard ayo.com
0 comments:
Post a Comment