Mwana
mkubwa wa kiume wa mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe amepatikana na
hatia ya kuua bila kukusudia na kupigwa faini ya dola 800.
Russell
Goreraza alimgonga na kumuua mwanamume mmoja ambaye hakutambuliwa
katika gari lake katika mji mkuu wa Harare manmo mwezi Februari.''Ninajuta na ningependa kuomba msamaha kwa kitendo hicho'', Kijana huyo wa miaka 31 aliimbia mahakama.
Hakimu huyo alisema kuwa aliamua kuifutilia mbali leseni ya kijana huyo na kumpatia hukumu ya kifungo cha jela lakini akabadilisha nia yake kutokana na majuto yake.
Douglas Chikwekwe amesema kuwa hatua kwamba Goreraza alitekeleza kitendo hicho kwa mara ya kwanza pia kuliathiri uamuzi wake.
Gallos Official Blog
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment