Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Msanii wa bongofleva aliethibitisha kupata Zero kwenye mtihani wa Form IV.

Msanii wa bongofleva aliethibitisha kupata Zero kwenye mtihani wa Form IV.

MziwandaNATION
Huwa ni mara chache sana utasikia staa au mtu maarufu kajitokeza au kakubali kuweka wazi kuhusu sehemu aliyowahi kuharibu au kufeli kwenye maisha.
Kwenye muziki wa bongofleva tunae Nuh Mziwanda ambaye pia ni boyfriend wa msanii Shilole…… Nuh ameongea ukweli wa moyoni kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Kwenye maisha yangu ninachojutia ni nilivyofeli mtihani wangu wa form IV nilipata Zero kabisa na sikufanya mitihani kama mitatu, yote hiyo ilitokea sababu ya muziki’
‘Nilikua mtoto mwenye akili sana na Mama yangu alikua anategemea nitakuja kuwa mtu flani mwenye elimu yake kwenye familia yetu na sio Mwanamuziki, nyumbani kwetu tuko watano na mimi ndio wa mwisho na nilikua nina akili sana kuliko wote na kuanzia la kwanza mpaka la saba nilikua sishuki kwenye Wanafunzi kumi bora‘ – Nuh
mziwandanation4 
Kwenye sentensi nyingine Nuh anamalizia >>> ‘Kupata Zero Form IV ni jambo ambalo linanifanya nijute sana mpaka sasa, ningekaza ningekua nafanya muziki huku nikisoma lakini nilivyojua maswala ya muziki tu nikaachana na Masomo, najutia…. nilikuja nikarudia tena mitihani na nikafeli, inaniuma sana… kama ninavyokosea kiingereza sio kwamba napenda, ni shule hamna’
Nuh amesema kuna uwezekano wa kurudi shule >>> ‘shule ni kitu muhimu haikataliwi, ni kitu poa unakuwa Mwanamuziki alafu una elimu yako… na muziki naudai sana ndio maana naukazania sababu ulinifanya nifeli shule’
Msikie Nuh Mziwanda hapa kwa kubonyeza playWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips