Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Kondomu Inayotambua Maambukizi ya Zinaa Kama Gonorea na Kasendwe Yazinduliwa

Kondomu Inayotambua Maambukizi ya Zinaa Kama Gonorea na Kasendwe Yazinduliwa

Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.
Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
''tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.

Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .
Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''
''Kwa hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''
null

Wavumbuzi hao wanasema kuwa hiyo ni mojawepo ya njia salama ya kubaini usalama penzi lenyu
Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.
Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa
"Ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu'' WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips