Mkufunzi
mpya wa timu ya Togo Tom Saintfiet amemshtumu nahodha wa timu hiyo
Emmanuel Adebayor kwa ukosefu wa nidhamu baada ya mshambuliaji huyo wa
Tottenham kushindwa kujiunga na kikosi hicho kwa wakati ufaao kwa mechi
ya ufunguzi ya kufuzu kwa kombe la Afrika wikendi ijayo.
''Nilimuona
siku ya jumatano na Ijumaa lakini hayuko hotelini'',Saintfiet
aliviambia vyombo vya habari mjini Lome siku ya ijumaa.Mkufunzi huyo kutoka Ubelgiji alikuwa akizungumza kabla ya kuondoka kuelekea Togo ili kushiriki katika mechi ya kirafiki na Ghana siku ya jumatatu.
''Ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa timu hii lakini siwezi kushirikiana nao iwapo hawako katika timu,ni lazima wawe na nidhamu kama wengine''.
Klabu ya Adebayor Tottenham ilimpatia likizo mara mbili msimu huu ili kurudi nyumbani na kusuluhisha maswala ya kibinafsi ambayo mshambuliaji huyo amelalamikia katika mitandao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment