Jack Warner amesema atafichua kila anachojua katika FIFA
Aliyekuwa
makamu wa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Jack Warner amesema
katika hotuba ya kushangaza aliyotoa katika runinga kwamba atafichua
kila anachojua kuhusu ufisadi katika shirikisho hilo.
Bwana Warner
ambaye alisema kuwa anahofia maisha yake pia amesema kuwa anaweza
kuwahusisha maafisa wa FIFA na uchaguzi mkuu katika taifa la Trinidad
and Tobbago mwaka 2010.Mmoja wa maafisa wakuu wa FIFA na shahidi muhimu Chuck Blazer alikubali kuchukua hongo.
Idara ya mahakama ya Marekani inadai kuwa watu 14 walioshtakiwa walikubali hongo ya zaidi ya dola milioni 150 katika kipindi cha miaka 24.
Gallos Official Blog
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment