Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Wolper Anaswa na Kigogo Mpya!

Wolper Anaswa na Kigogo Mpya!

Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti la risasi la leo, kigogo huyo ni mtu mwenye fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.


Chanzo hicho kilishusha data kuwa jamaa huyo ndiye aliyempangia Wolper nyumba ya kifahari iliyopo ushuani Mbezi-Beach jijini Dar.Huku akirusha picha za kimahaba za wawili hao, sosi wetu huyo alisema kuwa Jimmy ni ‘mtu f’lani hivi amazing’ kwa sababu anakata mkwanja kinoma.

Kama mtakumbuka kuna siku gazeti lenu mliandika kuwa Wema (Sepetu) na Wolper walilewa chakari kwenye pati ya ‘bethidei’ ya Petit Man, basi huyo kigogo ndiye aliyewafanyia kufuru na ile pati ilifanyika nyumbani kwake, Kinondoni-Manyanya (Dar),” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.

Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia ambazo gazeti hili linazishikilia zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.

Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, gazeti hilo lilimtwangia simu Wolper na kumsomea mashitaka yake juu ya mwanaume huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:

Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”

Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika ndiye huyo Jimmy. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips