Sitti Mtemvu Akiwa na Mdogo wake Ambae Watu walizusha ni Mtoto wake |
Amesema tuhuma hizo zilimuumiza sana hasa baada ya mdogo wake wa mwisho kutaniwa na wanafunzi wenzake wakidai kuwa amekuwa akiwadanganya Sitti, ni dada yake kumbe ni mama yake mzazi.
Amesema kuwa ilifika wakati akiwa anaenda kumchukua mdogo wake shuleni marafiki wa mdogo wake walikuwa wanamtania wakidai mdogo wake ni mtoto wa ‘bibi bomba’ wakimaanisha yeye jambo ambalo mdogo wake lilikuwa linamuumiza sana.
Ameongeza kuwa kuna kipindi mdogo wake alikataa kwenda shule kutokana na utani kuzidi pia magazeti kuandika kuwa Sitti, ana uhusiano na baba yake mzazi jambo ambalo lilimuathiri sana mtoto huyo.
Katika hatua nyingine Sitti alisema hausiki na hajasababisha kufungiwa kwa shindano la Miss Tanzania.
“Sijui kama nahusika na sijui kama sihusiki, sijaona sehemu ambayo wameandika imefungwa Miss Tanzania sababu ya Sitti, kwamba nahusika? Hapana, kama nilivyokwambia sidhani kama nahusika vitu vingi vinaweza kutokea kwa wakati mmoja.” alisema Sitti.
Pia Sitti aliyegoma kuzungumzia umri wake, alizikanusha tetesi za kutoa rushwa ya ngono kwa mwaandaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
“Hakuna uhusiano wowote kati yangu na Hashim Lundenga na hayo maneno yaliandikwa mengi kusema mimi na mtoto, ni maneno ya watu ambao walijisikia kama kunichafua.”
Sitti amewataka wadau na mashabiki wake kukitafuta kitabu chake cha ‘Chozi la Sitti’ ambacho ndani kimezungumzia mambo mbalimbali kuhusu maisha yake pamoja na changamoto alizopitia
0 comments:
Post a Comment