Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti la Risasi, ambacho kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray alipofika na kuharibu shughuli.
“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.
Baada ya kupata habari hiyo, gazeti hilo liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Davina.
“Jamani mi nafikiri nisizungumzie hilo tukio maana naona ni la aibu, si kitendo kizuri na kinaniumiza mno kwa maana ni udhalilishaji mno na kwa nini mtu akufanyie hivyo?,” alisema Davina. Simu ya Ray iliita bila kupokelewa. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment