Nimeishi na mke wangu kwa miaka mitano tukiwa na amani na furaha, lakini upendo ulianza kulegalega kuanzia mwaka jana mwezi wa kumi na mbili pale ambapo uume wangu ulipoanza kushindwa kusimama hivyo kutokidhi mahitaji ya kindoa kwa mke wangu, nimejaribu tiba za kila aina lakini sijapata tiba.
Mke wangu ananitishia kuniacha kwani anadai haoni thamani ya mimi kuwa naye na mbaya zaidi siku hizi akienda kwa kazi anachelewa kurudi, nikimuuliza anadai mara nilikuwa semina, mara tulikuwa na kikao na bosi, kwakweli jambo hili linaniumiza sana, imefikia kipindi natamani tuachane kwani imekuwa kero kwangu, moja ugongwa nilo nao unanivuruga na pili mke wangu amekuwa mbogo, haoni tena thamani yangu kwake.
Naomba msaada wenu WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment