Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi leo asubuhi katika kituo cha mabasi ubungo jijini Dar es Salaam baada ya madereva ambao wanaendesha mgomo kuanza kuwarushia mawe baadhi ya viongozi waliofika kwa ajili ya mazungumzo na madereva hao akiwemo mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda na mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga.
Akiongea na mtandao huu, Afisa kutoka chama cha kutetea
abiria, CHAKUA, bw, Gervas Lutaguzinda amesema kuwa madereva walianza
kuwarushia mawe viongozi hao baada kudai kuwa ahadi wanazozitoa sio za
msingi hivyo kutaka waziri mkuu afike eneo hilo.
Hata Hivyo Bw Lutaguzinda amesema kuwa hali kwa sasa
imetulia na viongozi hao wanaendelea na mazungumzo na madereva hao ili
kufikia muafaka wa tatizo hilo ambalo limefanya baadhi ya abiria kulala
kwenye magari tangu jana.
0 comments:
Post a Comment