Aidha amesema ni vyema wananchi wa Jiji la Arusha na maeneo mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, ili waweze kupiga kura na kuchagua wagombea wanaotaka kuongoza.
Lema amesema hata asipopiga kampeni za kutetea kiti hicho yeye bado ni mbunge na uchaguzi huu ataendelea kushinda kwani wagombea wanaopitapita kutangaza nia na baadhi yao kugawa unga, bila mboga anawafananisha na bendera zinazoendelea kupepea bila kuwa na mafanikio yoyote.
Amesema ni vyema wananchi wakajitokeza kuhakikisha daftari hilo la wapiga kura likitangazwa kufika mkoani Arusha, wanajitokeza kwa wingi kujiadikisha ili waweze kutumia haki yao siku ya uchaguzi na kuongeza idadi ya wabunge na madiwani wengi kupitia Chadema.
Lema amesema kwa jinsi anavyoona hadi sasa maandalizi ya uchaguzi mkuu yanasuasua, hivyo yawezekana daftari hilo likitangazwa kuhamia
mkoani Arusha siku zinaweza kuwa chache hivyo ni vyema wananchi wakawa makini, wakisikia daftari linapita mkoa fulani wajitokeze kwa wingi kujiandikisha, ili waweze kuchagua wabunge wengi kutoka Ukawa.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment