Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Maandamano Burundi yachukua Sura Mpya

Maandamano Burundi yachukua Sura Mpya

Serikali ya Burundi imewataka  waandamanaji katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura kusitisha maandamano yao dhidi ya hatua ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwezi ujao.

Serikali  imewapatia waandamanaji hao saa 48 kuondoa vizuizi walivyoweka katika barabara za mji huo,lakini hata hivyo inadaiwa maandamano yataendelea leo  siku ya jumapili.

Wanasiasa  wanasema kuwa bwana Nkurunziza anakiuka katiba kwa kuwania muhula wa tatu,lakini mapema wiki hii mahakama ya kikatiba nchini Burundi iliamua kuwa rais Nkurunziza ana haki ya kuwania muhula wa tatu.

Hadi sasa takriban watu 18 wameuawa tangu maandamano hayo yaanze wiki mbili zilizopita. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips