Akijibu tuhuma hizo Dr. Slaa amesema wazi kuwa Chadema na UKAWA hawapo tayari kupokea mafisadi kwani itakuwa ni kinyume kabisa na dhamira ya UKAWA ya kuwatumikia watanzania wanaotegemea mabadiliko makubwa.
"Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko na wameonyesha nia ya dhati kutuunga mkono, hatupo tayari kuchafuka na mafisadi" amesema Dr. Slaa
Kutokana na hali halisi ilivyo mdani ya CCM, chama hicho kinatarajiwa kukumbwa na mgogoro mkubwa kutokana na msuguano mkali wa makundi mawili makubwa yanayowania urais huku kundi hasimu na Lowassa likiungwa mkono na rais Kikwete.
Lowassa tayari ametoa hotuba huku akiainisha vipaumbele vyake ambavyo vinaenda kinyume kabisa na ilani ya CCM mwaka 2015-2020 jambo linalohashiria kuwa ndani ya chama hicho hali si shwari. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment