Habari kutoka duru za siasa za CCM zinadai kwamba CCM wamepanga kumtosa rasmi Lowasa kwenye mbio za urais ila watampoza kwa kumuahidi cheo cha uwaziri mkuu. Habari za kuaminika kutoka kada maarufu wa CCM anayehudumu katika ofisi ndogo ya Lumumba zinabainisha kwamba vikao vya "usuluhishi" kati ya kundi linalomuunga mkono Lowasa na wasuluhishi hao vimekuwa vikifanyika Dodoma na Dar ili kuweka mambo sawa.
"Tunataka tuingie kwenye uchaguzi tukiwa wamoja ndipo tutaweza kukabiliana na nguvu kubwa ya UKAWA. Wananchi wa sasa sio kama wa enzi hizo...hawadanganyiki! Ndio maana hata uamuzi wa adhabu dhidi ya makada waliofungiwa na chama kwa kuanza kampeni mapema tumeuahirisha kwa muda ili kujipanga vizuri.", Alisema.
Kufuatia uwoga wa kushindwa uchaguzi uliotanda ndani ya CCM, hadi sasa wameogopa kupuliza kipenga kwa makada kuanza kuchukua fomu kwa kuhofia kuibuka kwa makundi yanayoweza kukiangamiza chama.
MAONI YANGU
CCM msijidanganye kumpoza Lowasa huku mkijua kwamba mnampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment