Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Aunty Ezekiel na Kajala Masanja Wamseng'enya Wema Sepetu

Aunty Ezekiel na Kajala Masanja Wamseng'enya Wema Sepetu

MASTAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja, juzikati walikutana na kutumia muda wa takriban nusu saa (dakika 30) kumsengenya aliyekuwa shosti wao, Wema Sepetu.

Tukio hilo lilijiri  hivi karibuni kwenye Bustani za Ndoto Polepole zilizopo Bagamoyo, ambapo mastaa kibao walihudhuria sherehe ya Baby Shower ya Aunt, iliyokuwa imesheheni vituko kibao huku gumzo likiwa ni kutokuwepo kwa Wema.

Awali paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakimzungumzia Wema tena huku watu wengine wakisikia, kubwa likiwa kumshangaa kwa namna anavyotaka kila anayekuwa rafiki yake, awe adui wa maadui zake.Mjadala huo ulikuwa mkubwa, ambapo Kajala kuna wakati alimuuliza Aunt sababu ya Wema kutokuwepo eneo hilo ndipo alipompa mkasa mzima.

Mazungumzo hayo ya Kajala na Aunt yaliwafanya hata waalikwa wengine kumteta Wema, wakidai kuwa anatakiwa kujiangalia kwani ni staa ambaye hadumu na marafiki zake na mara nyingi wakiachana, huachana kwa ubaya.Ijumaa lilijaribu kuingilia mazungumzia hayo ili kujua kisa cha wao kutumia muda mwingi kumjadili Wema lakini wote waliishia kuguna kisha kuendelea na sherehe hiyo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips