Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » WEMA SEPETU: Kumuimba Msichana Uliyeachana naye ni USHAMBA wa Mapenzi

WEMA SEPETU: Kumuimba Msichana Uliyeachana naye ni USHAMBA wa Mapenzi

Staa wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu wasichana wanaoachana nao kimapenzi.

Wema amesema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi, wakiwalenga waliokuwa wapenzi wao.

Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekani mlikuwa mnafurahia wote mapenzi yenu, lakini mkiachana anakutungia nyimbo za kukuponda, hakuna neno la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’ alisema Wema.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kutoka studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini, kuna wimbo wa wasanii wawili waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo, ambao wanamalizia kurekodi wimbo unaodaiwa unamzungumzia mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips