Kama
ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya urembo utagundua kuwa wasichana
wengi wanofanya maonesho ya mitindo ya mavazi na masuala la urembo wana
maumbo madogo madogo hivi.. wengi ni wembamba, hivi umewahi kuona eti
mwanamitindo mnene hivi?
Bunge la Ufaransa limepitisha Sheria
inayopiga marufuku makampuni yanayojihusisha na masuala ya mitindo
nchini humo kutumia wasichana wembamba kupita kiasi.
Watu
wanaofanya kazi ya kuwatumia models wanatakiwa kuanzia sasa watumie
wasichana au wanawake ambao sio wembamba sana, ila wawe na wembamba
ambao ni salama kiafya, yoyote akienda kinyume ni faini ya Euro 75,000
hivi ambazo Bongo ni zaidi ya Mil. 140 pamoja na Mmiliki wa Kampuni
inayohusika kufungiwa kwa zaidi ya miezi sita.
Usishtuke na hii mtu wangu, nimepita
mitandaoni na kuona kumbe Israel iliweka Sheria hiyo pia mwaka 2013,
Italy na Spain wao walitengeneza kanuni ambazo zinasaidia pia kuzuia
kutumia wanawake wembamba sana na waliodhoofu.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment