Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , » Mchungaji Mbaroni kwa Kumchinja Mwanaye Adai "Nilioteshwa na Mungu, Mkuu wa majeshi Nimtoe Sadaka"

Mchungaji Mbaroni kwa Kumchinja Mwanaye Adai "Nilioteshwa na Mungu, Mkuu wa majeshi Nimtoe Sadaka"

DUNIA ina mambo! Mchungaji wa kanisa moja mjini Harare nchini Zimbabwe, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amekamatwa na polisi baada ya kukutwa akitaka kumuua mwanaye wa kumzaa kwa kumchinja na kisu shingoni, kitendo alichokifanya nyumbani kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mchungaji huyo ambaye hata hivyo hakueleweka ni wa kanisa gani, akiwa amevaa nguo zake za kichungaji, kanzu nyeupe yenye msalaba kifuani, alimchukua mwanaye huyo wa kiume na kuanza kumchinja ndani ya nyumba yake, kabla ya kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi, kupiga kelele za kuomba msaada.

Kwa mujibu wa mitandao, baada ya majirani kuingia ndani ya nyumba hiyo, walimkuta mchungaji huyo akiwa na kisu mkononi, ameloa damu huku kijana wake akiwa ameanguka chini akiugulia kwa maumivu makali.

Baada ya kuhojiwa sababu za kutaka kutoa roho ya mwanaye, mchungaji huyo alitoa majibu ya kushangaza;
“Nilioteshwa na Mungu, Mkuu wa majeshi. Alinitaka kumtoa sadaka mtoto wangu kama kweli nilikuwa na imani naye, sasa kwa sababu kila siku hufanya mambo yangu kwa kusikia sauti yake, nikaifuatisha. Ni kama Ibrahim alivyofanya katika Biblia.”

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kijana huyo alikuwa bado hajafariki na aliwahishwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu wakati mchungaji huyo ameendelea kuwa mikononi mwa polisi ambao wanamhoji kabla ya kufikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips