Jay
ameamua kuendelea kuonyesha ni jinsi gani amewekeza katika himaya ya
burudani duniani baada ya jana kuingia mkataba na kampuni mpya
inayojulika kwa jina la Tidal ambayo sasa atakuwa akinunua kazi za wasanii wengine na kuziuza kupitia kampuni hiyo.
Raper
huyo katika uzinduzi huo uliofanyika New York aliamua kuwashirikisha
wasanii wakubwa wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya muziki duniani
ambao ndio waanzilishi katika kampuni hiyo.
Wasanii hao ni pamoja na Alicia Keys, Arcade Fire’s Win Butler na RĂ©gine
Chassagne, Beyoncé, Daft Punk, Jack White, Jason Aldean, J. Cole, Kanye
West, Deadmau5, Madonna, Nicki Minaj, Rihanna, Calvin Harris, Chris
Martin na Usher.
Alicia
Keys ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kwa ufupi kuwa lengo la
kuungana ni kuhakikisha wanshirikiana kaika sauti moja na kuhakikisha
wanaleta mapinduzi katika historia ya muziki kwa manufaa ya mashabiki na
wasanii kwa ujumla.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment