Miongoni mwa taarifa zilizochukua Headlines katika taarifa ya Habari ya kituo cha ITV ni hii ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima ambae amefika kituo kikuu cha Polisi Dar kwa ajili mahojiano na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa kauli yenye maneno makali kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki, Askofu Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima
amesema maneno aliyoyatoa ni ya kumkemea kiongozi mwenzake wa kiroho
kwa madai ya kukiuka msimamo wa viongozi wenzie wa dini wa kukataa
Mahakama ya Kadhi.
“Baraza
la Maaskofu Tanzania waliamua kwa pamoja na wakasaini waraka kwa
pamoja, kwamba hawataki Mahakama ya Kadhi… lakini tukashangaa mwenzetu Askofu Pengo
aliyesaini na yeye anageuka sasa tukajiuliza kwa nini anageuka? mimi
kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee.. lakini nimeitwa na Polisi
sasa najiuliza niliyemkemea ni Polisi au nilimkemea nani?“ –Askofu Gwajima.
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii
kumezagaa picha za video zenye maneno ya kashfa kwenda kwa kiongozi wa
Kanisa Katoliki Askofu Kardinali Pengo jambo lililofanya jeshi la Polisi kumtaka afike kituoni kikuu cha Polisi kwa mahojiano.
Sikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha ITV kwa kubonyeza play hapa chini…WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment