Kaka wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aitwaye Methusela Gwajima amemtaka mdogo wake kwenda kumuomba radhi Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo kwa kutoa lugha ya kumkashifu.
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam,
Methusela alisema ameamua kutokufumbia macho kitendo cha ndugu yake
kumkashifu Pengo na kwamba anapaswa kujitathimini alipopotoka kwa
kumtukana kiongozi mkubwa wa kiroho kwani ni sawa na kuidhalilisha
familia nzima ya Ukoo wa Gwajima.
Alisema maneno yake ya kashfa ni dhahili ya kuwa hata ukoo
mzima umedhalilishwa hivyo familia ya Methusela Gwajima imemtaka
kuomba radhi mara moja.
Hata hivyo alisema kuwa yeye ni kada wa CCM hivyo amepata
usumbufu mkubwa tokea sakata hilo liibuke maana ndugu na marafiki
walioko nje ya nchi wamekuwa wakimuuliza kuhusiana na suala hilo hali
inayompa wakati mgumu kuwapatia majibu.
Alisema kashfa hizo hazina tija kwa taifa na haileti
uhusiano mwema baina ya madhehebu ya dini, bali yanachochea chuki,
uhasama, utengano na hasira kati ya wakristo kwa wakristo.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment