Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Watu 3 Wateketea Kwa Moto Baada ya Lori La Mafuta Kupinduka na Kuwaka Moto

Watu 3 Wateketea Kwa Moto Baada ya Lori La Mafuta Kupinduka na Kuwaka Moto

Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam.

Mwandishi wetu  alishuhudia kikosi cha zimamoto ambao walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka.

Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.

Waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.

Nao wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleza jinsi tukio lilivyotokea ambapo wananchi wamelalamikia eneo hilo kuwa limekuwa na matukio mengi ya ajali na hivyo kuomba serikali kuona umuhimu wa kuweka vituo vya zimamoto katika eneo hilo kwani magari ya zimamoto yalichukua muda mrefu kufika kwenye eneo la tukio kutokana na umbali mrefu.

Nae afisa mkaguzi msaidizi wa kikosi cha zima moto Hamadi Dadi ameeleza walivyopata taraari za ajali wametumia muda mrefu kufika katika eneo la tukio ingawa wametumia muda mrefu kuzima moto huo kutokana na mafuta yaliyokuwa yakivuja.

Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na askari walionekana muda wote kwenye eneo la tukio.

----------
If you love somebody, let them go, for if they return, they were always yours. And if they don't, they never were.
Khalil Gibran
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips