Habari kutoka kwa chanzo kilicho karibu na wanandoa hao wanaoishi wilayani Temeke, kinasema kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya watu hao, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kusaliti, jambo linaloonyesha wakati wowote ndoa yao inaweza kusambaratika.
“Jamaa hayuko ‘peace’ kabisa na ndoa yake, yaani kila siku ni mgogoro, wife wake anamshutumu mshkaji kuwa msaliti kwa wanawake wengine na mke naye anatuhumiwa hivyohivyo ili mradi hakuna amani kabisa.
Inaonekana kuna tatizo kubwa,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Gazeti hili halikuweza kuwapata wanandoa hao kutokana na simu zao kutopatikana, lakini wakati linakwenda mitamboni, lilipata taarifa za kufikishwa mahakamani kwa Mheshimiwa Temba, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua, kitendo alichokifanya kwa Godfrey Deogratius anayemtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkeweWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment