Wasanii hao wamekamata nafasi za kwanza wiki hii kwenye top ten za chart za muziki wa Afrika katika vituo vikubwa viwili vya runinga.
Diamond Platnumz amekamata nafasi ya kwanza kwenye African Top 10 ya Trace International na wimbo wake Ntampata Wapi.
Naye AY amekamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Africa Rox Countdown ya Soundcity kwa wimbo wa ‘Touch Me’ aliowashirikisha Sean Kingston na Ms Triniti.
Wasanii wengine wa Tanzania waliopo kwenye chart hiyo ni pamoja na Shaa na Navy Kenzo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment